Atabatu Abbasiyya inaomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya Majlisi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Mzungumzaji wa Majlisi hiyo alikuwa ni Sayyid Muhammad Naji, ameongea kuhusu hadhi ya Mtume (s.a.w.w), na upekee wake ukilinganisha na mitume wengine, ukizingatia yeye ndio mtume wa mwisho.

Akaongea kuhusu historia yake tukufu, iliyojaa mazingatio na mafunzo mengi yanayotakiwa kufanyiwa kazi, sambamba na kuangazia namna alivyoweza kuvumilia na kubadilisha watu.

Majlisi itadumu kwa muda wa siku tatu, Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba kamili ya kuomboleza msiba huu, kwa kufanya Majlisi na kutoa mihadhara ya Dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: