Atabatu Abbasiyya yafungua usajili wa ziara ya Mtume (s.a.w.w) kwa niaba.

Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua mlango wa kusajili ziara ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa niaba, kwenye malalo yake takatifu katika mji wa Madina na kuhitimishwa na ziara maalum kwenye malalo ya kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s).

Ziara hiyo inasimamiwa na idara ya teknolojia na mitandao chini ya kitengo cha Habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Watu wote watakao jisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, watafanyiwa ziara na waumini wanaoishi Madina, na Najafu watafanyiwa ziara na watumishi wa Atabatu Abbasiyya, watafanyiwa ziara maalum na swala ya rakaa mbili kwa nia ya kukidhiwa haja na kurahisishiwa mambo.

Kwa yeyote anayependa kufanyiwa ziara ajisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: