Rais wa kitengo hicho Mhandisi Alaa Jaburi amesema “Ataba tukufu inabeba mazuwaru wanaokwenda kwenye malalo ya kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), kutoka vituo vya nje ya mji hadi katikati ya mji wa Najafu katika mnasaba wa kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imekamilisha maandalizi ya kubeba mazuwaru, imetuma gari (100) kwa ajili ya kubeba mazuwaru kutoka na Kwenda katika malalo tukufu kwa kushirikiana na idara za hapa mkoani”.
Kundi kubwa la waumini kutoka ndani na nje ya Iraq, huja kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w) kwenye malalo ya mtoto wa Ammi yake Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu.