Kitengo cha utumishi kinaendelea kusafisha Barabara zinazoelekea Atabatu Abbasiyya tukufu.

Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, wanaendelea kusafisha Barabara zinazoelekea kwenye haram takatifu, baada ya kumaliza ibada ya ziara ya Arubaini.

Kazi ya kusafisha Barabara zinazoelekea Ataba tukufu inaendelea baada ya kumaliza ziara ya Arubaini, kwa ushiriki wa kitengo cha usafi.

Kazi ya usafi imehusisha uwanja wa mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye kituo cha utumishi, kwa namna ambayo itaendana na utukufu wa sehemu hii na mazuwaru, sambamba na kuhusisha Barabara zingine nyingi.

Kitengo kimeanza kufanya kazi toka mwanzoni mwa mwezi wa Safar, kimetoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: