Idara ya Masayyid katika Atabatu Abbasiyya hufanya kazi tofauti katika kuhudumia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake watukufu.
Idara inafanya kazi za utoaji wa huduma, maelekezo, husafisha haram tukufu, kusafisha dirisha la kaburi tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s), kuongoza Majlisi na Mawakibu Husseiniyya za waombolezaji zinazo shiriki kwenye harakati tofauti za Atabatu Abbasiyya.
Idara ya Masayyid hushiriki pia kwenye vikao vya kijamii, hususan vinavyo husu kutatua mizozo ya kikoo na kijamii kwa ujumla, kufanya ziara kwa niaba ya kila anayehitaji huduma hiyo kupitia mtandao wa Alkafeel.
Idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inaumuhimu wa pekee, kwani wamerithi kazi hiyo kutoka kwa mababu zao.