Chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w).
Majlisi hiyo imehudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani, makamo wake Dokta Nawaal Aaid Almayali, viongozi wa vitengo na walimu.
Majlisi ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu kutoka kwa msomaji wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Najafu, chini ya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Almayali.
Kisha akapanda mimbari Mheshimiwa Shekhe Abdillahi Dujaili, akaongea kuhusu historia ya Mtume na namna alivyo itoa jamii katika giza la ujinga na kuwatia katika nuru ya elimu, kwa kufundisha Dini ya kiislamu na misingi ya ubinaadamu.
Majlisi ikahitimishwa kwa tenzi na mashairi yaliyoeleza kifo cha Mtume (s.a.w.w) na dhulma alizofanyiwa kutoka kwa jamii isiyojua utukufu wake na watu wa nyumbani kwake (a.s).