Zaidi ya sahani (3000) za chakula zimetolewa na maukibu ya Majmaa-Ilmi kwa mazuwaru wa Najafu.

Maukibu ya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu imegawa zaidi ya Sahani (3000) za chakula kwa mazuwaru wa malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) wakati wa ziara ya Nabawiyyah.

Maukibu inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Kiongozi wa idara ya utoaji wa huduma Sayyid Samiri Sharbah amesema “Maukibu imehudumia mazuwaru wanaotembea kwa miguu Kwenda katika malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) kufanya ziara ya Nabawiyya mwezi (28) Safar siku ya kumbukizi ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.

Akaongeza kuwa “Kuanzia jioni ya jana hadi asubuhi ya leo maukibu imegawa zaidi ya sahani (3000) za chakula, nusu tani ya matumba mbalimbali, juisi na vinginevyo”.

Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imeandaa maukibu kwa ajili ya kutoa huduma tofauti kwa mazuwaru ikiwa ni sehemu ya ratiba ya mradi wa Qur’ani kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: