Mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, siku ya Alkhamisi mwezi ishirini na nane Safar, wameomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) mbele ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala.
Barabara zinazoelekea katika malalo mbili takatifu na malango ya kuingia katika mji wa Karbala, yameshuhudiwa makundi
makubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya taifa.
Kumbuka kuwa siku chahe zilizopita, mji mtukufu wa Karbala ulipokea mamilioni ya watu kutoka kila sehemu ya dunia waliokuja kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kuonyesha mapenzi yao kwa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya ilifanya kila iwezalo katika kuhudumia mazuwaru, ilihakikisha ulinzi na usalama kwao, upatikanaji wa huduma za afya, chakula, maji na mambo mengine.