Idara ya maelekezo ya Dini katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa, imetoa huduma kwa Zaidi ya watu (35000) wakati wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka 1445h.
Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shami amesema “Wanufaika wa huduma zetu kuanzia mwezi kumi Safar yadi mwezi ishirini walizidi watu (35000)”.
Akaongeza kuwa “Huduma zilikuwa baina ya masomo ya Fiqhi, Aqida, Akhlaq, Qur’ani na Malezi, mihadhara (83) imetolewa na khitima (16) zimegawiwa kwa mazuwaru huku halaqa (145) za maelekezo ya kidini zikifanywa, aidha kulikuwa na ratiba maalum ya watoto kwenye vituo vyote vya Atabatu Abbasiyya”.
Harakati za idara zimefanywa kwa kutumia lugha mbili, kiarabu na kifarsi sambamba na matembezi ya mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) wanaoelekea Karbala, tumefanikiwa kupokea idadi kubwa ya watu wanaokuja kufanya ziara.