Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani amepokea mwanafunzi aliyefanya vizuri kwenye masomo yake, Sefu Dini Saad.
Sayyid Sistani amempokea mwanafunzi Sefu Dini Saad akiwa na wazazi wake baada ya kushinda kwa kiwango cha juu kwenye mitihani ya darasa la sita, Pamoja na kuwa na maradhi ya kupooza toka udogoni mwake.
Sayyid Sistani amepongeza juhudi kubwa ya kijana huyo katika masomo pamoja na changamoto ya maradhi aliyonayo.
Akamuambia kuwa “Kufaulu kwako ni somo muhimu kwa watu wote kuwa hakuna kinachoweza kumzuwia mwanaadamu katika Maisha yake pale atakapokuwa na nia ya kweli na kutokata tamaa, akamtaka aendelee vyema katika masomo yake, aidha ameipongeza familia yake kwa kushikamana naye na kumtia moyo katika masomo”.