Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w).
Kiongozi wa idara Sayyid Taghrid Tamimi amesema “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na ziara ya Mtume (s.a.w.w), halafu ukafuata muhadhara wenye anuani isemayo (Maqamaati Nabii -s.a.w.w- katika dua ya asubuhi) iliyotolewa na Mhadhiri Nagham Muhammad”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara ulijikita katika kueleza tofauti ya muongozo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mitume wengine (a.s) na kuonyesha utukufu wa Mtume wa mwisho mbele ya mitume wote wa Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Mwisho wa Majlisi zikasomwa kaswida na tenzi za kumpa pole imamu wa zama Mahadi msubiriwa (a.s).