Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ridhwaa (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Mussa Ridhaa (a.s).

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala na kuhudhuriwa na wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na kundi la mazuwaru.

Mhadhiri wa Majlisi Sayyid Muhammad Naaji amesema “Atabatu Abbasiyya huhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) kwa kufanya Majlisi za kuomboleza, ikiwemo hii ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Mussa Ridhwaa (a.s) mwezi ishirini na tisa Safar, Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu”.

Akaongeza kuwa “Tumeeleza historia ya Imamu (a.s) na dhulma alizofanyiwa wakati wa uhai wake sambamba na elimu na uchamungu wake, na umuhimu wa kuchukua somo na mazingatio katika uhai wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: