Atabatu Abbasiyya yahitimisha Majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Atabatu Abbasiyya imehitimisha Majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w) ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Majlisi hizo zilisimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu.

Mhadhiri wa Majlisi Shekhe Ibrahim Naswirawi amesema “Majlisi ilipambwa na mhadhara wa kidini kuhusu historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na nafasi yake katika kufundisha Dini ya Kiislamu, hakika Mwenyezi Mungu alimtuma kuwa rehema kwa walimwengu wote na kukamilisha kazi zilizofanywa na Mitume na Manabii”.

Akaongeza kuwa “Majlisi nyingi zimefanywa kuomboleza kumbukumbu ya kifa cha Mtume (s.a.w.w).

Akasema: “Majlisi zimehudhuriwa na watu wengi miongoni mwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: