Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wamefanya kitendo cha kiibada katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Sayyid Ali Mamitha mmoja wa watumishi wa kitengo cha uhusiano katika Ataba amesema “Kitendo cha kiibada kimefunguliwa kwa ziara maalum ya Abulfadhil Abbasi (a.s), iliyofuatiwa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa)”.
Akaongeza kuwa “Kitendo hicho hufanywa mara mbili kwa wiki, siku ya Jumanne na Alkhamisi, hii ni mara ya kwanza katika mwezi wa Rabiul-Awwal”.
Akaendelea kusema “Watumishi wa Atabatu Abbasiyya hukumbuka matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kwenye kisimamo hicho ambacho hushiriki kundi kubwa la mazuwaru waliopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.