Kikosi cha Abbasi kimefanya mkutano wa kutathmini utendaji wake katika ziara ya Arubaini.

Kikosi cha Abbasi (a.s) kimefanya mkutano wa kutathmini huduma kilizotoa wakati wa ziara ya Arubaini.

Mkuu wa kikosi hicho Shekhe Maitham Zaidi amesema “Tumefanya kikao cha kujadili na kutathmini huduma tulizotoa wakati wa ziara ya Arubaini kwa mazuwaru watukufu, miongoni mwa huduma ni ulinzi, chakula na afya”.

Akaongeza kuwa “Katika kikao hicho, tumepokea maoni na mapendekezo ya viongozi na wadau, sambamba na kujadili mikakati ya utoaji wa huduma katika miaka ijayo”, akasema “Kikosi cha Atabatu Abbasiyya kilitoa huduma tofauti wakati wa ziara ya Arubaini”.

Akasema “Kikao kinalenga kuangalia ukamilifu na upungufu kwa lengo la kuweka mikakati ua maboresho katika miaka ijayo na kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: