Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amesema kuwa utaratibu wa kuendeleza watumishi, umejenga uwezo wa kiidara katika Ataba tukufu.
Ameyasema hayo wakati alipohudhuria jaribio la kupokea watumishi watakaopewa mafunzo ya kujengewa uwezo katika mambo ya kiidara.
Akasema: “Utaratibu wa kujenga uwezo wa kiidara kwa watumishi unapewa kipaombele sana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi”, akabainisha kuwa “Huu ni mradi wa pekee katika Ataba za Iraq, unalenga kujenga uwezo wa watumishi wa Ataba tukufu katika mambo ya kiidara”.
Akaongeza kuwa “Utaratibu huu unaongozwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, umepata mwitikio mkubwa kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wamejitokeza kujenga uwezo wao katika mambo ya kiidara”.