Wizara ya elimu imepongeza kazi nzuri inayofanywa na jumuiya ya Al-Ameed katika sekta ya elimu.

Wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu kupitia muwakilishi wake Dokta Haidari Abdu Dhwahadi imepongeza kazi nzuri inayofanywa na jumuiya ya Al-Ameed katika sekta ya elimu.

Muheshimiwa muwakilishi wa wizara amekabidhi waraka wa shukrani na pongezi kwa rais wa idara ya jumuiya ya Al-Ameed, katika waraka huo amesifu kazi nzuri ya tafiti za kielmu iliyofanywa kwa zaidi ya miaka mitatu.

Waraka huo ni kielelezo cha mafanikio ya jumuiya katika shughuli za kielmu.

Kumbuka kuwa Al-Ameed ni jumuiya ya kielimu iliyo anzishwa chini ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu kwa mujibu wa kanuni za jumuiya za kielimu namba (55) ya mwaka (1981m), namba yake ya usajili ni (BT2-7199 katika 24/7/2019m).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: