Shirika lililoratibu maonyesho na kongamano la kielimu, limekipa tuzo chuo kikuu cha Al-Ameed kulingana na weledi wake katika tafiti za kielimu.
Shirika limewezesha shughuli za maonyesho na kongamano la kielimu lililofanywa kwenye uwanja wa maonyesho ya kimataifa jijini Baghdad kwa kushirikiana na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, vimetolewa vyeti vya ubora kwa taasisi zilizo kamilisha vigezo chini ya kauli mbiu isemayo (Usomaji.. kufanyia kazi fikra na mustaqbali), miongozi mwa waliopewa vyeti hivyo ni chuo kikuu cha Al-Ameed.
Vyeti vimekabidhiwa na Dokta Haidari Abdu Dwahadi muwakilishi wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, na kupokewa na muwakilishi wa chuo kwenye maonyesho hayo Dokta Jasim Muhsin Sultani.