Chuo kikuu cha Alkafeel kimeanzisha kituo cha udaktari na famasia.
Kituo hicho kimeanzishwa baada ya kupata kibali rasmi kutoka wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, sambamba na kupatikana kwa maabara, mitambo ya kisasa, wakufunzi weledi na bobezi.
Kituo kinahusika na tafiti za kitabibu na famasia kulingana na mahitaji ya taifa, aidha ni kitovu cha tafiti za kiafya katika chuo.
Chuo kikuu cha Alkafeel kinahakikisha upatikanaji wa mahitaji yote muhimu yanayo endana na ubora wa kielimu, kwa lengo la kupata kizazi bora chenye uwezo mkubwa wa kuhudumia jamii.