Balozi wa Misri nchini Iraq amepongeza kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu.

Balozi wa Misri nchini Iraq Sayyid Walidi Muhammad Ismaili, ameipongeza Atabatu Abbasiyya na ukarimu wa raia wa Iraq katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Ataba tukufu alipokutana na makamo rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Jalukhani, aliye eleza uzowefu wa Atabatu Abbasiyya katika mambo tofauti na mafanikio yaliyofikiwa.

Balozi wa Misri baada ya kufanya ziara kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mazingira mazuri ya kiroho, akasema kuwa “Ataba imefanya kazi kubwa ya ujenzi katika maeneo yanayozunguka malalo takatifu”.

Akafafanua kuwa “Atabatu Abbasiyya inamchango mkubwa katika kufanikisha ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu ikiwemo ziara ya Arubaini”.

Balozi wa Misri amesifu mapokezi mazuri aliyopewa na wahudumu wa Atabatu Abbasiyya, aidha amepongeza uwezo mkubwa walionao Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: