Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa shindano la kidini kwa watu wanaotembelea tawi lake linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu jijini Baghdad awamu ya ishirini na nne.
Kiongozi wa tawi la Atabatu Abbasiyya katika maonyesho hayo Sayyid Muhammad Aaraji amesema “Shindano linafanywa kwa kuchagua maswali na kuyajibu, maswali yanahusu maudhui za kidini, kielimu na kitamaduni, mtu anaejibu vizuri anapewa zawadi ya vitabu na majarida ya Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa “Shindano lilifanywa siku ya kwanza ya ufunguzi wa maonyesho, na yataendelea kwa muda wa siku kumi” akasema kuwa “Shindano linalenga kujenga uwelewa wa kidini na kitamaduni katika jamii, sambamba na kujenga moyo wa kushindana kielimu na kushajihisha kusoma na kufanya tafiti katika turathi za Ahlulbait (a.s)”.