Kituo cha taaluma Alkafeel chini ya chuo kikuu cha Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya warsha kwa watumishi wa taasisi ya Imamu Swadiq (a.s) katika mkoa wa Baabil kuhusu namna ya kufanyia kazi jukwaa la Siraaj.
Mhadhiri wa warsha Ustadh Wasaam Ali Alkhuzai amesema “Warsha imejikita katika kueleza utendaji wa program katika sehemu mbili, kwanza kiidara. Taarifa za walimu, wanafunzi, ratiba za masomo, mahudhurio na mengineyo, sehemu ya pili inahusisha utumaji wa mihadhara kwa wanafunzi, utoaji wa majaribio kwa njia ya mtandao, kutoa alama na kuwasiliana baina ya mwalimu na mwanafunzi”.
Akaongeza kuwa “Kupitia jukwaa hili, kituo kinalenga kutoa elimu kwa njia ya mtandao katika taasisi za kielimu kwa lengo la kuporesha elimu na kuendeleza uwezo wa wanafunzi”.
Mkufunzi wa lugha ya kiengereza katika shule ya Imamu Swadiq (a.s) Ustadh Hussein Muhammad amesema “Kwa mwaka wa pili mfululizo tumekuwa tukifanya warsha za kutambulisha program ya jukwaa la Siraaj, warsha ya mwaka huu imekua kubwa tofauti na miaka mingine”, akasema kuwa “Utumiaji wa program hii unaleta maendeleo makubwa katika kuboresha elimu kwa wanafunzi”.