Miongoni mwa mradi wa mimbari za Qur’ani.. Majmaa-Ilmi imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika mji wa Baabil.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani ikiwa ni sehemu ya mradi wa mimbari za Qur’ani.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Muhammad Maamuri akafuatia msomaji Swalahu Ibadi.

Ikahitimishwa kwa muhadhara uliotolewa na Dokta Haidari Shalaa, ameongea kuhusu nafasi ya Qur’ani tukufu sambamba na mbinu za kutafakari aya na kutambua ta-awili yake na sababu za kushushwa kwake.

Maahadi hufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani na utoaji wa mihadhara katika mikoa tofauti ya Iraq kwa lengo la kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: