Kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimejadiliana na taasisi za afya zilizo chini ya wizara ya afya kuhusu namna ya kushirikiana katika ufundishaji.
Hayo yamesemwa wakati mkuu wa kitivo cha udaktari Dokta Saamir Maki, msaidizi wake Dokta Ali Naajih Al-Awaadi na Dokta Haidari Swahibu Almayali walipotembelea vituo vya taasisi za afya vilivyo chini ya wizara ya afya, kwa lengo la kujenga uwezo wa wanafunzi.
Kitivo cha udaktari katika chuo cha Alkafeel kinafanya kila kiwezalo katika kuboresha uwezo wa wanafunzi wake na kuwafanya kuwa madaktari bora katika jamii.