Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeandaa kikao cha usomaji wa Qur’ani katika Maqaam ya Swahibu Zamaan (a.f) kwa ushiriki wa wanafunzi wake.
Kikao hicho ni muendelezo wa mradi wa kiongozi wa wasomaji unao simamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Wafuatao wameshiriki katika usomaji wa Qur’ani kwenye kikao hicho (Muhammad Hussein Hani, Ali Akbaru Mustwafa, Muhammad Hisham Ni’imah na Muhammad Mahadi Abbasi) huku muongozaji wa hafla akiwa ni Sajjaad Abbasi.
Mradi unahusisha masomo ya hukumu za usomaji wa Qur’ani, kufanya warsha, kutoa mihadhara ya kidini na kufundisha mwenendo bora na maadili ya kibinaadamu.