Majlisi itadumu kwa muda wa siku tatu kuanzia siku ya Ijumaa, inasimamiwa na idara ya wahadhiri katika Ataba tukufu.
Majlisi inafanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mhadhiri alikuwa Shekhe Jafari Ibrahimi, ameongea kwa ufupi kuhusu historia ya Imamu (a.s) na msimamo wake katika kutatua matatizo ya jamii.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na qaswida za kuomboleza zilizo amsha huzuni katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s), kutoka kwa waimbaji mahiri Khadhar Abbasi na Mula Muhammad Muutamadi, huku mazingira yakiwa yamejaa majonzi na huzuni.