Idara ya Fatuma binti Asadi imeanza kuranya ratiba yake ya kila wiki (Ulizeni wanaojua).

Idara ya Fatuma binti Asadi inayohusika na masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kutekeleza ratiba wake ya kila wiki iitwayo (Ulizeni wanaojua) ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Ratiba imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na muhadhara wa kifiqihi kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) uliokuwa unasema (Mambo tofauti katika wakfu za Ataba)”.

Akaongeza kuwa “Program inalenga kueneza misingi ya Qur’ani, Dini na maadili, imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanawake, wamekuwa washiriki na wahudhuriaji wazuri”.

Idara ya Fatuma binti Asadi inalenga kueneza uwelewa wa Dini kwa watoto kupitia mladi wa (Ulizeni wanaojua), imeandaa ratiba maalum ya watoto iitwayo (Uwanja wa watoto), watoto wanaelimishwa na kujengewa moyo wa kushindana baina yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: