Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya semina maalum kuhusu matumizi ya vifaa vya elektronik kwa kushirikiana na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Semina iliyofanywa kwa kushirikiana na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani, imehusisha majaji wa Maahadi watakao shiriki kwenye ujaji wa shindano lijalo la kitaifa”.
Akaongeza kuwa “Semina imehusisha kuwafundisha majaji namna ya kutumia vishikwambi (tablet) zitakazotumika kwenye ujaji wa shindano lijalo”.
Akaendelea kusema “Wamefundishwa namna ya kutumia program maalum za kutumia kwenye ujaji, zinazo rahisisha upatikanaji wa matokeo ya washiriki”.