Ataba mbili tukufu Askariyya na Abbasiyya, zimeendesha mradi wa kufundisha usomaji sahihi kwa mazuwaru na waombolezaji wa Imamu Hassan Askariy (a.s) katika mji wa Samaraa.
Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Jawadi Nasrawi amesema “Maahadi ya Qur’ani tukufu kwa kushirikiana na Daarul-Qur’ani ya Atabatu Askariyya, tumefanya mradi wa kufundisha usomaji sahihi kwa mazuwaru wa maimamu wawili Askariyyaini (a.s) katika kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askari (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Jumla ya vituo vinne vya kufundisha usomaji wa Qur’ani tukufu vimefunguliwa katika eneo la Haram takatifu na sehemu zinazo zunguka Haram, kwa lengo la kufundisha mazuwaru usomaji sahihi wa surat Fat-ha na baadhi ya sura fupi ambazo hutumika mara nyingi katika swala pamoja na nyeradi za swala”.
Akaendelea kusema “Mradi huu umefanywa kwa mwaka wa tano chini ya ushirikiano wa Ataba mbili tukufu, jumla ya walimu (19) wameshiriki”, akasema “Mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa ziara ya Arubaini ndio yametusukuma kufanya mradi huu hapa Samaraa, kama sehemu ya kuhudumia mazuwaru katika kuomboleza msiba huu”.