Mhadhiri wa Husseiniyya Shekhe Imaadu-Dini amesema kuwa, Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s).
Akaongeza kuwa “Majlisi imeangazia historia ya Imamu Hassan Askariy (a.s) na mafanikio makubwa aliyopata katika kurekebisha umma wa kiislamu, sambamba na kubainisha utukufu wake kupitia maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.
Wahudhuriaji wakatuma rambirambi zao kwa Imamu Mahadi (a.f), maraajii watukufu na umma wa kiislamu.