Waumini wanafanya ziara na kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) katika mji wa Samaraa.

Kundi kubwa la waumini linaomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Samaraa.

Muandishi wetu amesema kuwa kundi kubwa la mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq wamekuja Samaraa kufanya ziara na kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), akabainisha kuwa; mji umeshuhudia kushindikizwa kwa jeneza la kuigiza sawa na lile la Imamu Hassan Askariy (a.s) na lilikuwa na washiriki wengi.

Akaongeza kuwa “Ulinzi na usalama umeimarishwa katika mji wa Samaraa toka siku za nyumba kwa ajili ya kuhakikisha mazuwaru na mawakibu wanapata huduma bora, bila kusahau kuna mawakibu zinagawa chakula na vinywaji bure kwa mazuwaru”.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake tofauti ilianza kutoa huduma siku tano zilizopita, kwa kushirikiana na Atabatu Askariyya, huduma tofauti zimekuwa zikitolewa kwa mazuwaru wa mamlalo ya Askariyaini (a.s) katika mji wa Samaraa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: