Raudhat Ahbaabul-Kafeel chini ya Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuwa kensho siku ya Jumatatu itaanza kupokea mabinti wenye umri wa miaka (4 – 5).
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Raudha yetu imeanza kusajili mabinti sambamba na kuwapatia mahitaji yote ya lazima katika masomo yao, tumekuwa tukifanya hivi kila mwaka”.
Akasema “Maahadi inawakufunzi mahiri na waliobobea katika mambo ya watoto, kumbuka kuwa usafiri wa kwenda na kurudi bure umeandaliwa”.