Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s).
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na ziara ya Imamu, halafu likafuata igizo lenye anuani isemayo (Kilio cha Samaraa) kutokana na dhulma za Bani Abbasi kwa Imamu Hassan Askariy (a.s).
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma Qaswida na Duau-Faraj ya Imamu wa zama (a.f).