Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye ufunguzi wa sanamu la Sayyid Haidari Alhilliy katika mji wa Baabil.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye ufunguzi wa sanamu la mshairi wa Ahlulbait (a.s) Sayyid Haidari Alhilliy katika mkoa wa Baabil.

Hafla ya ufunguzi wa sanamu imefanywa katika kumbukizi ya miaka (141) toka kufa kwake, na kuhudhuriwa na ujumbe kutoka kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kibinaadamu na kiislamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla imehudhuriwa na wanachuoni, wakazi wa mji wa Hilla na maeneo ya Jirani bila kusahau wanafamilia ya Sayyid Alhilliy.

Ushiriki huu ni sehemu ya kuwakumbuka watu muhimu waliochangia kwa kiasi kikubwa kujenga utamaduni wa mji wa Hilla miaka ya nyuma.

Sayyid Alhilliy ni mfano mzuri katika sekta ya mashairi ya kiitikadi na kuwapenda Ahlulbait (a.s), bado qaswida zake zinasikika kila mahala zinakofanywa Majlisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: