Ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria tawi la wanawake imeandaa warsha elekezi kuhusu shughuli za kimali.

Ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa warsha kuhusu shughuli za kimali katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s).

Mkufunzi alikuwa ni Sajaad Hussein Abdurahim, na washiriki ni idara tofauti za wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Warsha inalenga kutambua matumizi na mgawanyo wa kazi pamoja na utaratibu wa ajira na mishahara kwenye idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Wasimamizi wa warsha wameandaa muongozo maalum kwa njia ya mtandao utakaotumika siku chache zijazo, kwa lengo la kupata mafanikio makubwa katika shughuli za kimali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: