Ofisi ya Marjaa-Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani imetoa tamko kuhusu tukio la moto katika wilaya ya Hamdaniyya mkoani Nainawa.
Ifuatayo ni nakala ya tamko:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu
(Hakika sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea)
Marjaa-Dini mkuu anatuma salam za rambirambi kwa huzuni na majonzi makubwa kufuatia tukio la moto katika wilaya ya Hamdaniyya uliosababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kujeruhiwa, tunatoa pole kwa familia za waathirika na tunamuomba Mwenyezi Mungu awape subira na awaponye haraka majeruhi, hatuna hila wala nguvu ispokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mkuu na mtukufu.
11 Rabiul-Awwal 1445h.
Ofisi ya Sayyid Sistani – Najafu Ashrafu.