Mkufunzi wa semina kutoka kitengo cha Dini Shekhe Faaiq Alghanimi amesema “Semina imehusisha somo la Fiqhi, Aqida, Akhlaq pamoja na kujadili changamoto mbalimbali mbele ya washiriki 100”.
Akabainisha kuwa “Semina imepambwa na kuonyesha utajili wa Dini kwenye sekta ya utamaduni, washiriki wametoa ushirikiano mkubwa na wamefuatilia kwa karibu mihadhara yote iliyotolewa”.
Akaendelea kusema kuwa “Semina imefanywa kwenye majengo ya Shekhe Kuleini, mihadhara mbalimbali inatolewa kwa watumishi wapya wa Ataba na itadumu kwa muda wa siku tano”.