Pembezoni mwa shindano la vizito viwili.. Majmaa-Ilmi inafanya warsha ya kubainisha namna ya kuandika Msahafu mtukufu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya warsha ya kubainisha namna ya kuandika msahafu mtukufu kwa kundi la waandishi wa kiiraq.

Warsha hiyo inasimamiwa na kituo cha uchapishaji wa msahafu mtukufu chini ya Majmaa.

Rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali amesema “Warsha inalenga kubainisha namna ya kuandika msahafu mtukufu kwa hati yenye muonekano mzuri kama ilivyo kwenye misahafu mingine, kwa kushiriki waandishi wa kiiraq na waarabu”.

Akaongeza kuwa “Warsha hiyo inawashiriki (150) miongoni mwa waandishi wa kiiraq na kutoka kwenye nchi za kiarabu”.

Shindano la zawadi ya vizito viwili linahusu uandishi wa msahafu mtukufu, linasimamiwa na kituo nalo ni la pekee katika ulimwengu wa kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: