Wamekuja kutoka nje ya Iraq.. Majmaa-Ilmi inawapa zawadi wageni wa shindano la Thaqalaini la hati ya msahafu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imewapa zawadi wageni wa shindano laThaqalaini la hati ya msahafu mtukufu waliokuja kutoka nje ya Iraq.

Amepewa zawadi mtaalamu wa hati Dokta Muhsin Abadi kutoka Iran na Sayyid Abbasi Mussawi kutoka Baharain.

Hafla ya utowaji wa zawadi imehudhuriwa na makamo wa taaluma Dokta Liwaau Hassan Atwiyya na mkuu wa kituo cha uchapishaji wa msahafu Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi.

Watalam wa hati kutoka na Iran na Baharain, wamepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya yakiwemo mashindano na semina zinazo endeshwa na Ataba kwa lengo la kueneza maarifa ya Qur’ani na kuifanya jamii ijali mambo yanayohusu Qur’ani tukufu.

Jumla ya watu (47) wameshiriki kwenye shindano la msahafu, ambalo ni sehemu ya matunda ya zawadi ya vizito viwili, program inayo endeshwa na kituo cha uchapishaji wa msahafu mtukufu chini ya Majmaa-Ilmi, tumechagua watu kumi miongoni mwao, watakao shiriki kwenye uandishi na kila mmoja ataandika juzu tatu za Qur’ani tukufu kwa hati ya Naskhi, ambayo ndio hati inayotumika katika Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: