Kiongozi wa idara ya Habari katika Maahadi bibi Israa Akarawi amesema “Maahadi imefanya hafla ya kuhitimisha mashindano ya kitaifa awamu ya sita kwa ushiriki wa mahafidhu kutoka mikoa (9) ya Iraq, na kulikuwa na washindi (9)”.
Akaongeza kuwa “Washindi walikuwa makundi matatu (kundi la waliohifadhi Qur’ani yote), (kundi la waliohifadhi juzuu 20) na kundi la waliohifadhi juzuu 15), katika kila kundi kulikuwa na washindi watatu”.
Akaendelea kusema “Hafla ya kufunga mashindano imepambwa na visomo tofauti kutoka kikosi cha Nab’u-Juud, Baraaimu-Naiim Aljuud, na kisomo maalum kutoka kwa mwanafunzi mwenye ulemavu, aidha imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kike”.