Idara ya Fatuma binti Asadi inayojihusisha na masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla maalum ya kuadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w).
Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Idara imeandaa hafla maalum ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mbora wa walimwengu (s.a.w.w) kupitia ratiba ya kila wiki (Ulizeni wanaojua) ambayo hutekelezwa ndani ya Ataba tukufu.
Akaongeza kuwa “Hafla ilikuwa na muhadhara uliotolewa na mmoja wa watumishi wa maktaba ya Ummul-Banina (a.s), amebainisha utukufu wa Mtume (s.a.w.w), zikafuata qaswida kuhusu mazazi ya Mtume mtukufu”.
Akaendelea kusema “Hafla imehudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), Idhaa ya Alkafeel imeshiriki kwa kuendesha shindano kuhusu Mtume (s.a.w.w) na washindi wakapewa zawadi za kutabaruku”.
Idara ya Fatuma binti Asadi inayojishughulisha na masomo ya Qur’ani huadhimisha matukio maalum yanayo muhusu Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), ikiwa ni sehemu ya kufanyia kazi kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu).








