Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, raia wa Iraq ni wabunifu na wanaweza kujenga taifa wakipata mazingira muwafaka.
Muheshimiwa Sayyid Swafi katika maneno yake ya ufunguzi kwenye hafla ya kuwapongeza wakufunzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed amesema: “Tunatoa pongezi kubwa kwenu kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume (s.a.w.w) na Imamu Swadiq (a.s), mmekiwezesha chuo kupata ufaulu mkubwa kuanzia kitivo cha udaktari, udaktari wa meno, uuguzi, famasia na kwenye vitengo vingine vyote vya kielimu”.
Akafafanua kuwa “Atabatu Abbasiyya imeweka kipaombele kwenye sekta ya elimu, kupitia chuo kikuu cha Al-Ameed, Alkafeel na taasisi za kimalezi zilizo chini ya vyuo hivyo, tumeweza kuonyesha kwa vitendo namna tunavyojali sekta ya elimu”.
Akasisitiza umuhimu wa kuanzishwa chuo kikuu cha Al-Ameed, Alkafeel na taasisi za kimalezi na kielimu katika Atabatu Abbasiyya, akasema kuwa “Chuo ni nyumba ya wote, kuna ulazima wa kufanya kila kitu kinachoweza kuinua kiwango cha elimu, ukizingatia kuwa elimu huanzwa wala haimalizwi, kila inapoboreshwa huwa na matokeo mazuri zaidi”.
Akafafanuwa kuwa “Sekta ya elimu na malezi humuathiri kila mtu katika taifa, kuna athari zingine sio rahisi kuziona, huenea katika mfumo wa elimu na malezi katika taifa”.
Muheshimiwa akaendelea kusema kuwa “Tunaamini kuwa raia wa Iraq wana akili ya ubunifu, wanaweza kuleta maendeleo iwapo wakipewa mazingira wezeshi katika utekelezaji wa majukumu yao, jambo hilo ndio lililotusukuma kufanya kazi kwa bidii ya kuziwezesha taasisi za elimu”.
Muheshimiwa Sayyid Swafi akatoa wito wa kuendelea kufanya juhudi katika utekelezaji wa majukumu ya ufundishaji na ulezi kwa kujenga misingi ya maadili mazuri kwa wanafunzi, kwani chuo ni mradi wa (kielimu na kimalezi) wala huwezi kutenganisha kimoja wapo na kingine.