Katika Hospitali ya Alkafeel.. katibiwa mgonjwa aliyekuwa na tatizo la kupooza mishipa ya sauti.

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumfanyia upasuaji mgonjwa aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la kupooza mishipa ya sauti.

Daktari bingwa wa upasuaji wa masikio, pua na koo, Dokta Naadhim Imrani amesema “Mgonjwa anaumri wa miaka arubaini, alikuwa amepooza mishipa ya sauti, kwa sababu ya kuongezeka kwa ukubwa wa koromeo na kusababisha kupata tatizo la sauti, hivyo imepidi afanyiwe upasuaji kwa ajili ya kurekebisha koromeo na mfumo wa sauti”.

Akaongeza kuwa “Tumefanya upasuaji kwa umakini wa hali ya juu, tumerekebisha koromeo kwa kutumia njia maalum”, akabainisha kuwa “Aina hiyo ya upasuaji ni ngumu sana, lakini kutokana na uwepo wa madaktari mahiri na vifaa-tiba vya kisasa vimesaidia kufanikisha upasuaji huo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: