Akasema kuwa “Wanafunzi wa shule za Al-Ameed mwanzoni mwa mwaka mpya wa masomo, wameweza kuwatambua walimu wao na kutambuana wao kwa wao, jambo hili litawasaidia katika safari ya masomo, aidha wameanza safari ya masomo wakiwa na ari kubwa inayowapa matumaini ya kufikiwa malengo yao”.
Akaongeza kuwa “Kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi anahimiza umuhimu wa kuongeza juhudi na kupatikana mafanikio tuliyo ahidi katika shule za Atabatu Abbasiyya”.
Akabainisha kuwa “Baada ya kumaliza msimu wa masomo wa mwaka jana, tulianza maandalizi ya msimu wa masomo ya mwaka huu (2023 – 2024)”.
Akaendelea kusema “Idara ya shule za Al-Ameed ilifanya semina na warsha mbalimbali za kuwajengea uwezo walimu wakati wa likizo” akasisitiza kuwa “Hakika kuna umuhimu mkubwa wa kutengeneza kizazi cha watu wenye maadili mazuri na elimu, wenye uwezo wa kujenga taifa letu kipenzi”.