Majmaa-Ilmi imeadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w).

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w) kwa kufanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika mji mkuu wa Baghdad.

Hafla imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa.

Hafla imefanywa kwenye msikiti na husseiniyya ya -Maimamu wawili- katika eneo la Khatibu Zirai, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Amiri Aadil, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu.

Ukafuata ujumbe kutoka kwa mhadhiri wa msikiti Shekhe Haidari Rikabi, akatoa pongezi ya mazazi hayo matukufu, hafla ikapambwa na sauti ya msomaji wa Qur’ani Ahmadi Bahadeli kisha yakafuata mashairi yaliyosomwa na Ali Dhahabi na mwisho ikasomwa Duaau-Faraj.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: