Program ya Mahdawiyya imepata muitikio mkubwa.

Program ya Mahdawiyya inayoendeshwa na kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, imepata muitikio mkubwa katika harakati zake.

Program hiyo inasimamiwa na kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo.

Mtafiti kutoka kwenye kituo hicho Sayyid Muhammad Hassan amesema “Program ilianza katikati ya mwezi wa Shabani mwaka 1443h, inaendelea na harakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuendesha mashindano kila wiki na program za usomaji ambazo zimepata muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki, hakika umekuwa msaada mkubwa katika mambo ya kitamaduni”.

Akaongeza kuwa “Kituo bado kinaendelea na program za kimtandao, miongoni mwake ni program ya Mahdawiyya inayoendeshwa na idara ya masomo na tafiti katika kituo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: