Hafla imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, wajumbe wa kamati kuu Sayyid Jawadi Hasanawi, Dokta Abbasi Dida Mussawi, baadhi ya marais wa vitengo, mkuu wa mkoa wa Karbala Sayyid Naswifu Khatwabi, viongozi wa kijamii na mazuwaru.
Rais wa kitengo cha Habari na utamaduni katika Ataba tukufu Sayyid Aqiil Yaasiri amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s) mbele ya mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wahudumu wa Ataba na mazuwaru watukufu”.
Akaongeza kuwa “Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu kutoka kwa msomaji wa Ataba mbili Sayyid Haidari Jalukhani, ukafuata ujumbe kutoka kwenye uongozi mkuu wa Ataba tukufu, kisha wakapanda kwenye mimbari washairi na waimbaji wa qaswida, wakasoma tenzi na kuimba qaswida”.
Akafafanua kuwa “Hafla kama hiyo imefanywa pia ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), hafla imehitimishwa kwa kutembelea nyumba ya wazee katika mji wa Karbala na kuwapa zawadi”