Mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Dida amesema, hakika tumeadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa kubainisha mwenendo na ujumbe wake uliomtoa mwanaadamu kwenye giza na kumtia kwenye nuru.
Mussawi katika ujumbe aliotoa kwa vyombo vya Habari wakati wa maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s) amesema “Atabatu Abbasiyya huadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na matukio mengine yote yanayofungamana na Dini, kwa lengo la kubainisha ujumbe wa Mtume (s.a.w.w) uliowatoa watu kwenye giza na kuwatia kwenye mwanga, hakika lengo la Mtume (s.a.w.w) ni kuwafanya watu wafuate muongozo wa Mola wao mtukufu”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya inaadhimisha mazazi ya Mtume (s.a.w.w) kwa sababu yeye ndiye msingi wa kushushwa wahyi na msingi wa matukio yote wa kidini ambayo hufanywa na Atabatu Abbasiyya”.
Akaendelea kusema kuwa “Hakika Mtume (s.a.w.w) ndiye msingi wa utatuzi wa changamoto zote anazopata mwanaadamu katika zama hizi”.