Katika maadhimisho ya wakweli wawili.. watumishi wa Atabatu Abbasiyya wanapokea mazuwaru kwa kuwapa pongezi na mauwa.

Watumishi wa idara ya masayyid kutoka kitengo cha uangalizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wamepokea mazuwaru na kuwapongeza kwa kuwapa zawadi na mauwa.

Sayyid Badri Mamitha mmoja wa watumishi wa idara ya masayyid amesema “Jambo hili ni sehemu ya harakati zilizoandaliwa na Atabatu Abbasiyya katika maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Wahudumu wa Ataba tukufu wamesimama milangoni kupokea mazuwaru na kuwapa zawadi ya mauwa na pipi, kama sehemu ya kuwaonyesha umuhimu wa tukio hili” akabainisha kuwa “Jambo hilo limepokelewa vizuri na mazuwaru watukufu na wametoa pongezi nyingi”.

Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake vyote hufanya maadhimisho yanayohusu Ahlulbait (a.s) ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: