Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya mbora wa walimwengu.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya mbora wa walimwengu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Hafla imepambwa na igizo lenye anuani isemayo (Imezaliwa Nuru), lililofanywa na kikosi cha maigizo, kimeonyesha mambo tofauti muhimu yanayohusu mazazi matukufu ya Mtume.

Hafla ikahitimishwa kwa kufanya mashindano na kugawa zawadi kwa washindi, sambamba na kuwazawadia kikosi cha igizo kama sehemu ya kuwapongeza kwa kuandaa igizo zuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: